ICJ YAONYA KUHUSU GHASIA KABLA YA UCHAGUZI WA 2027
Takribani mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027, wasiwasi umeibuka kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa ghasia za kisiasa na matumizi ya vijana kama magenge ya kuzua vurugu.
Tume ya Kimataifa ya Wanasheria (ICJ) imeonya kuwa kutumia vijana walio katika hali ngumu kiuchumi kuzua vurugu, pamoja na kuongezeka kwa matamshi ya chuki, kunaweza kuchochea ukosefu wa utulivu nchini kuelekea uchaguzi.
Huduma ya Kitaifa ya Polisi kwa upande wake imekataa madai kwamba ndiyo kiini cha tatizo, ikisema sababu za ghasia za kisiasa zinahusisha changamoto pana za kijamii na kisiasa zinazohitaji kushughulikiwa kwa pamoja.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































