GOR MAHIA KUKUTANA NA PYRAMIDS KATIKA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Kocha wa Gor Mahia Charles Akonnor amesema yuko tayari kukabiliana na Pyramids FC ya Misri katika raundi ya kwanza ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisema mchezo huo utakuwa kipimo muhimu kwa kikosi chake kipya.
Gor Mahia itakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza mjini Nairobi kati ya Septemba 4 na 6, kabla ya kusafiri hadi Misri kwa mechi ya marudiano wiki moja baadaye. Mshindi wa jumla ataingia raundi ya pili na kukutana na mshindi kati ya El Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini na Heegan FC ya Somalia.
Akonnor amesema licha ya ukubwa wa changamoto hiyo, anaiona pia kama fursa ya kupima maendeleo ya kikosi chake tangu alipochukua usukani wa mabingwa hao akisisitiza kuwa hana nia ya kupoteza na analenga kujenga timu yenye ushindani mkubwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































