#Football #Sports

RONALD ARAUJO AJIUNGA NA LIVERPOOL KWA MKOPO

Beki wa kati wa Uruguay Ronald Araujo amejiunga na Liverpool kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Barcelona.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya Uhispania, Liverpool itagharamia mshahara wa Araujo na ina chaguo la kumnunua kwa euro milioni 55 mwishoni mwa kipindi cha mkopo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Hansi Flick, huku kijana wa Uhispania Pau Cubarsí akiwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Barcelona.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *