#Local News

LEE  KINYANJUI AWASUTA VIONGOZI

Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Lee Kinyanjui, amewataka viongozi waliochaguliwa kuacha kulalamika hadharani katika majukwaa ya umma na badala yake kutumia nafasi zao za uongozi kutatua changamoto zinazowakabili Wakenya.

Akizungumza katika mahojiano kwenye televisheni moja humu nchini  Kinyanjui amewatetea viongozi wanaohudumu serikalini na kupinga dhana kwamba kufanya kazi chini ya serikali ya sasa humfanya mtu kuwa mbaya au asiye na maadili.

Kauli yake inajiri wakati ambapo siasa katika eneo la Mlima Kenya zimepamba moto, huku viongozi wa upinzani wakizidi kuikosoa serikali ya Kenya Kwanza katika matukio ya mazishi, mikutano ya kanisa na mikusanyiko mingine ya kijamii.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *