#Football #Sports

PSG YATWAA SUPER CUP, YAENDELEA KUTAWALA ULAYA

Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Paris Saint-Germain wameendeleza ubabe wao baada ya kuifunga Aston Villa 2-1 na kutwaa taji la UEFA Super Cup mjini Salzburg katika Mechi ambayo ilichezeshwa na mwamuzi wa Somalia Omar Artan

Khvicha Kvaratskhelia na Désiré Doué walifunga mabao ya PSG, huku kijana wa Aston Villa Brian Madjo akiandikisha bao katika mechi yake ya kwanza kwa klabu hiyo.

Ushindi huo umeifanya PSG kutetea taji la Super Cup walilolitwaa mwaka uliopita, baada ya kuifunga Tottenham Hotspur kwa mikwaju ya penalti.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *