#Local News

MUNGATANA: WABUNGE WAMEGEUKA MAWAZIRI WADOGO

Seneta wa Kaunti ya Tana River Danson Mungatana amewakosoa wabunge kwa kile anachosema ni kuipa kipaumbele Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (CDF) kuliko masuala mengine ya kitaifa.

Mungatana amesema wabunge huwa na misimamo tofauti kuhusu masuala ya kitaifa lakini wanapofika suala la CDF huwa tayari hata kuzuia bajeti ya taifa ili kuhakikisha fedha hizo zinapatikana.

Amesema wabunge wameanza kujiona kama watendaji wadogo wa serikali, wakizingatia zaidi namna ya kutumia karibu Shilingi bilioni 200 katika maeneo yao ya ubunge kuliko kutekeleza majukumu yao ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *