#Local News

MATIANG’I AITAKA KENYA IEPUKE SIASA ZA MATUSI

Mgombea urais wa Jubilee Dkt Fred Matiang’i ametoa wito wa umoja na kuheshimiana nchini kuelekea uchaguzi mkuu, akiwataka viongozi kukomesha utamaduni wa kutukanana katika siasa.

Matiang’i amesema viongozi wanapaswa kujenga siasa zinazowaunganisha Wakenya badala ya kutumia lugha ya matusi na kauli zinazoweza kuongeza migawanyiko wakati wa uchaguzi.

Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani pia amesema yuko tayari kuiongoza Kenya, akisema amepitia majaribio mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi na kufanikiwa katika majukumu aliyowahi kupewa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *