#Football #Sports

FERRAN TORRES AJIUNGA NA PSG KWA €50 MILIONI

Paris Saint-Germain imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Barcelona Ferran Torres kwa ada inayofikia euro milioni 50, huku makubaliano kati ya klabu hizo yakikamilishwa.

Torres, ambaye alionyesha kiwango bora katika fainali ya Kombe la Dunia, ameamua kuhamia Paris baada ya kuonyesha wazi kuwa PSG ndiyo ilikuwa chaguo lake la kwanza.

Uhamisho huo umekamilika baada ya mazungumzo ya klabu hizo kufikia hatua za mwisho kwa siku kadhaa, huku Torres sasa akitarajiwa kuanza sura mpya katika maisha yake ya soka PSG.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *