#Local News

RAIS RUTO AHUDHURIA TAMASHA YA MUZIKI BUNGOMA

Rais William Ruto amehudhuria hafla ya kilele cha mashindano ya 98 ya muziki kwa shule za msingi, sekondari na vyuo katika Ikulu Ndogo ya Kaunti ya Bungoma.

Hafla hiyo imewaleta pamoja wanafunzi kutoka taasisi mbalimbali za elimu nchini walioshiriki katika mashindano hayo ya muziki, huku washiriki wakionyesha vipaji vyao katika nyimbo na maonyesho ya kitamaduni.

Mashindano hayo yanalenga kukuza vipaji vya wanafunzi katika muziki na sanaa, pamoja na kuimarisha utamaduni na ubunifu miongoni mwa vijana kupitia shughuli za ziada za masomo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *