WAJUMBE WA ODM WAKUTANA NAIROBI
Zaidi ya wajumbe 200 wa Chama cha ODM wamekutana jijini Nairobi katika juhudi za kuimarisha chama hicho kwa kuwapokea wanachama wapya.
Viongozi hao wa ODM wamesema hatua hiyo inalenga kupanua wigo wa chama na kuongeza nguvu yake katika maeneo mbalimbali huku wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.
Mkutano huo pia unalenga kuwahamasisha wanachama kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama na kuimarisha mikakati ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































