ODM IKO IMARA, NYONG’O
Kaimu kinara wa chama cha ODM ambaye pia ni gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o, amewataka viongozi wa chama hicho kusalia waaminifu chamani, na kuwakumbusha kwamba wana jukumu la kuwatumikia wananchi.
Akizungumza jijini Kisumu, Nyong’o amesisitiza umuhimu wa kuimarisha usawa kwenye chama hicho cha chungwa, huku akitoa hakikisho kwamba chama hicho kitasalia imara licha ya Raila Odinga kuteuliwa kusimamia bara la Afrika.
Gavana huyo amezungumza katika mkutano wa hadhara kwa mara ya kwanza tangu akabidhiwe uongozi wa chama hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































