4 WAFARIKI KWENYE AJALI MIGAA, NAKURU
Watu 4 wamepoteza uhai papo hapo huku mwingine akijeruhiwa katika eneo la Migaa kaunti ya Nakuru kwenye barabara kuu ya Nakuru-Eldoret baada ya lori lililokuwa likisafirisha kuni kugongana ana kwa ana na lori jingine lililokuwa likisafirisha nyanya.
Kulingana na chifu wa Migaa Zachary Monari, watatu kati ya waliofariki walikuwa kwenye lori lililokuwa likisafirisha kuni na mwingine kwenye lori jingine.
Majeruhi anatibiwa katika hospitali moja eneo la Salgaa, wakazi wakilalamikia ongezeko la ajali eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































