FAMILIA KADHAA MAKUENI ZAOMBOLEZA VIFO VYA JAMAA ZAO
Familia kadhaa katika eneo la Kibwezi, Kaunti ya Makueni, zinaomboleza baada ya watu saba kufariki katika ajali ya barabarani iliyotokea Ijumaa Agosti 14, 2026.
zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika ajali hiyo huku manusura wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Familia za waliofariki sasa zimeanza maandalizi ya mazishi huku ndugu na marafiki wakiomboleza vifo hivyo. Tukio hilo limezua tena wasiwasi kuhusu usalama wa barabara na umuhimu wa kuchukua tahadhari ili kupunguza ajali na vifo barabarani.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































