LSK: VIONGOZI WANAOHUSIKA NA GHASIA WAWAJIBISHWE
Chama cha Wanasheria nchini LSK kimeapa kuwawajibisha maafisa wa serikali watakaobainika kuhusika na ghasia za kisiasa na matumizi ya makundi ya vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Rais wa LSK Charles Kanjama amesema chama hicho kiko tayari kuanzisha taratibu za kisheria na kikatiba dhidi ya maafisa hao iwapo ushahidi wa kutosha utathibitisha kuhusika kwao.
Kanjama amesema LSK inaweza kufanikisha kuondolewa mamlakani kwa maafisa wa serikali watakaopatikana na hatia ya kuhusika na ghasia, akisisitiza kuwa uwajibikaji lazima utegemee ushahidi thabiti na mchakato wa kisheria.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































