ICHUNG’WAH NA NYORO WAZOZANA BUNGENI BAADA YA KUONDOKA UDA
Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro wamezozana vikali Bungeni kufuatia uamuzi wa Nyoro kuondoka katika chama tawala cha UDA.
Mzozo huo umeibua madai ya upendeleo katika mgao wa bajeti huku Nyoro akitangaza kujiunga na People’s Party of Kenya na kuikosoa serikali kwa kushindwa kutimiza ahadi zake.
Nyoro pia ameishutumu serikali kwa madai ya kufadhili makundi ya vijana kuvuruga Wakenya, huku mzozo huo ukiongeza dalili za mgawanyiko wa kisiasa ndani ya muungano unaoongoza serikali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































