OBIRI NA KIPRUTO WALENGA KUTETEA MATAJI NEW YORK MARATHON
Wakenya Hellen Obiri na Benson Kipruto watarejea katika mbio za New York Marathon 2026 kutetea mataji yao, huku mashindano hayo yakisherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa njia yake maarufu inayopita mitaa mitano ya New York.
Obiri alitwaa taji lake la pili mwaka uliopita kwa kuvunja rekodi ya miaka 22 ya mbio hizo baada ya kutumia saa 2 dakika 19 na sekunde 51, huku ushindi wa tatu ukimweka katika orodha ya magwiji waliotwaa taji hilo mara tatu.
Kipruto naye atakutana na ushindani mkali akiwemo Mkenya Geoffrey Kamworor, mshindi mara mbili, na Abdi Nageeye wa Uholanzi, huku Kipruto akiwa bingwa mtetezi baada ya ushindi wake wa kusisimua katika mbio za mwaka 2025.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































