#Local News

OWALO: KENYA BADO HAIJAKOMAA KISIASA BAADA YA MIAKA 30

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali Eliud Owalo amesema inasikitisha kuwa zaidi ya miongo mitatu tangu Kenya kuingia katika mfumo wa vyama vingi, baadhi ya watu bado hawajaelewa umuhimu wa ushindani mzuri wa kisiasa.

Owalo amesema ushindani wa kisiasa unapaswa kuwa sehemu ya demokrasia na si sababu ya kuleta uhasama, chuki au migawanyiko miongoni mwa wananchi.

Ametaka viongozi na wafuasi wa vyama mbalimbali kuheshimu misimamo tofauti ya kisiasa na kuruhusu ushindani wa haki na wa amani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *