#Local News

GACHAGUA KUELEKEA MURANG’A SIKU MOJA BAADA YA NYORO

Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua leo anatarajiwa kufanya ziara katika Kaunti ya Murang’a huku mvutano wa kisiasa ukizidi kushika kasi kuhusu mwelekeo wa eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Gachagua anatarajiwa kuzindua ofisi ya DCP mjini Murang’a saa tano na nusu asubuhi kabla ya kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kangari na Kandara katika ziara yake.

Ziara hiyo inajiri siku moja baada ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kuwataka wakazi wa Murang’a kumpokea Gachagua.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *