#Local News

SAA YA UCHAGUZI 2027 YAANZA RASMI

Saa ya kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027 imeanza rasmi, huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, ikiweka wazi kanuni zitakazosimamia safari hiyo ya kisiasa kuanzia usajili wa wapiga kura hadi kampeni na upigaji kura.

Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Edung Ethekon, amesema Tume hiyo imechapisha Tangazo la Gazeti la Serikali nambari 13497, hatua inayoweka rasmi utekelezaji wa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi pamoja na Sheria ya Makosa ya Uchaguzi.

Hatua hiyo sasa inawaweka vyama vya kisiasa, wagombea watarajiwa na wadau wengine chini ya mfumo wa kisheria utakaosimamia uchaguzi wa 2027, huku taratibu za uteuzi wa wagombea, kampeni, makosa ya uchaguzi na maandalizi ya kura zikiwa sehemu ya ratiba hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *