#Local News

OBADO AOMBA MAHAKAMA KUMPA  ADHABU NYEPESI KWA SABABU ZA AFYA

Aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado ameiomba Mahakama Kuu imzingatie kwa kumpa adhabu nafuu, ikiwemo kifungo kisicho cha gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya Sharon Otieno.

Katika ripoti ya uchunguzi wa kijamii kabla ya kutolewa kwa hukumu iliyowasilishwa mahakamani leo, Obado ametaja umri wake, hali yake ya kiafya pamoja na muda mrefu uliochukuliwa kukamilisha kesi hiyo kuwa sababu zinazopaswa kuifanya mahakama kuzingatia kumpunguzia adhabu.

Wakati wa mahojiano na maafisa wa urekebishaji tabia, Obado aliendelea kukana kuhusika katika mauaji ya Sharon Otieno, licha ya kukiri kuwa wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *