#Rugby #Sports

KCB YAINGIA DRIFTWOOD IKIWA NA MORALI BAADA YA KUTETEA TAJI LA KABEBERI

Mabingwa wa Kabeberi Sevens KCB wanaelekea mashindano ya Driftwood Sevens jijini Mombasa wakiwa na imani ya kutwaa taji lingine baada ya kutetea ubingwa wao mwishoni mwa wiki.

KCB iliifunga Strathmore Leos 14-12 katika fainali ya Kabeberi, huku kocha Andrew Amonde akisema ushindi huo umeonyesha uimara wa kikosi chake licha ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika Dala Sevens.

KCB imepangwa katika Kundi B pamoja na Uganda Sevens, Kisumu RFC na Blak Blad, huku Amonde akiamini uwezo wa wachezaji wake kupambana hadi mwisho utawasaidia kutetea nafasi yao katika mashindano hayo ya Mzunguko wa Saba wa Taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *