#Local News

KINDIKI ASISITIZA KUTOBANDUKA MADARAKANI

Naibu wa Rais Kithure Kindiki amesisitiza kuwa hawezi kuondolewa madarakani akisema nafasi yake inalindwa na katiba akikumbusha jinsi Rais William Ruto alivyobaki madarakani licha ya msukosuko wa kisiasa wakati akiwa naibu wa Rais  Uhuru Kenyatta

Kindiki ameonekana kumlenga mutangulizi wake Rigadhi Gachagua aliyeondolewa madarakani kupitia muchakato wa  kumng’atua mwaka 2024

Akizungumza katika kaunti ya Tharaka Nithi alipokutana na maafisa wa chama cha UDA katika ngazi ya vituo vya upigaji kura Kindiki amesema wapo tayari kuajibishwa kutokana na ahadi walizotoa kwa wakenya katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *