AJALI 33 ZAUA WATU 40 NCHINI KATIKA SIKU 20
Angalau watu 40 wamefariki na wengine 180 kujeruhiwa katika ajali 33 za barabarani zilizoripotiwa nchini katika siku 20 za kwanza za Agosti, kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya.
Takwimu hizo zinaonyesha ongezeko kubwa ikilinganishwa na taarifa ya awali iliyotolewa mapema mwezi huu ambapo watu 31 walifariki na 75 kujeruhiwa vibaya katika ajali 23 ndani ya siku 13 za kwanza za Agosti.
Katika siku saba zilizofuata pekee, ajali nyingine saba na vifo tisa vilirekodiwa huku idadi ya waliojeruhiwa ikiongezeka zaidi ya mara mbili, hali inayoibua wasiwasi kuhusu usalama wa barabarani nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































