MATIANG AILAUMU SERIKALI KUTOKANA NA GHASIA HOMA BAY
Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Dakta Fred Matiang ameishtumu serikali kwa madai ya kutumia vurugu kuwa silaha ya kisiasa ya kujilinda madarakani
Akizungumzia ghasia zilizoshuhudiwa kwenye mkutano wa viongozi wa vugu vugu la linda mwananchi katika kaunti ya Homa Bay Matiang ambaye ni naibu kiongozi wa chama cha Jubilee amesema hakuna namna vurugu hizo zingetokea bila serikali kuwa na taarifa za awali.
Kulingana na Matiang mashambulizi dhidi ya wanachama wa linda mwananchi yaalipangwa mapema akisema mwenendo wa baadhi ya maafisa wa usalama unaibua maswali kuhusu uwezekano wa serikali kuhusika na ghasia hizo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































