#Football #Sports

ARTETA: ZUBIMENDI HAONDOKI ARSENAL

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesisitiza kuwa kiungo Martin Zubimendi haondoki klabuni hapo akimtaja kama mmoja wa wachezaji muhimu zaidi katika kikosi chake.

Arteta amesema Zubimendi alikuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Arsenal msimu uliopita, akisema mchango wake ulikuwa mkubwa katika kuisaidia timu kufikia nafasi nzuri kuelekea mwisho wa msimu.

Kocha huyo amesema bila mchango wa Zubimendi Arsenal isingefikia kiwango ilichofikia katika wiki za mwisho za msimu, akisisitiza kuwa mchezaji huyo bado ni sehemu muhimu ya mipango yake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *