#Football #Sports

INTER MILAN YAONGEZA PRESHA KUMTWAA CURTIS JONES

Inter Milan inapanga kuwasilisha ofa mpya kwa kiungo wa Liverpool Curtis Jones, ambaye amekuwa chaguo lao kuu katika safu ya kiungo tangu Januari.

Mawasiliano zaidi yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya Inter kuzungumza tena na wawakilishi wa Jones, huku ofa hiyo mpya ikiwa haihusiani na mchezaji mwingine yeyote kuondoka klabuni.

Uhamisho huo sasa unategemea makubaliano kati ya Inter Milan na Liverpool, huku klabu hiyo ya Italia ikisalia na nia ya kumsajili Jones kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *