#Local News

NYORO: PPK SIO MRADI WA SERIKALI

Kiongozi wa chama cha PPK, Ndindi Nyoro, amesema chama hicho bado ni sehemu ya Muungano wa Upinzani na kimejikita katika kuimarisha nguvu za upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027, akikanusha madai kuwa kinaelekea kujiunga na chama cha  UDA.

Akizungumza jijini Nairobi alipowapokea zaidi ya wajumbe 30, Nyoro amesema lengo lao ni kujenga muungano wenye nguvu wa kumpinga Rais William Ruto katika uchaguzi ujao.

Aidha, Nyoro ameunga mkono wito wa viongozi wa upinzani wa kuitaka ICC kuchunguza madai ya kuhusika kwa serikali katika kuongezeka kwa vurugu na vitendo vya magenge nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *