#Football #Sports

AL HILAL YATOA OFA YA €45M KUMSAJILI OLLIE WATKINS

Al Hilal imewasilisha rasmi ofa ya jumla ya euro milioni 45 kwa Aston Villa kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Ollie Watkins, kiasi hicho kikijumuisha malipo ya ziada.

Watkins anaripotiwa kuwa tayari kuhamia klabu hiyo ya Saudi Arabia, lakini uamuzi wa mwisho sasa uko mikononi mwa Aston Villa baada ya awali kukataa majaribio mawili ya kumsajili.

Al Hilal sasa imeweka ofa rasmi mezani huku ikisubiri majibu ya Aston Villa kuhusu uwezekano wa kukamilisha uhamisho wa Watkins .

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *