#Athletics #Sports

KIPYEGON KUKOSA SEHEMU YA MSIMU WA 2026 KISA JERAHA

Bingwa mara nne wa dunia wa mita 1,500 Faith Kipyegon anatarajiwa kusitisha mashindano kwa msimu uliosalia wa 2026 baada ya kufichua kuwa jeraha la misuli ya nyuma ya paja alilopata Mei limemlazimu kujiondoa.

Kipyegon amekuwa akipambana kurejesha kiwango chake cha kawaida katika mashindano mawili ya mwisho ya Diamond League, huku jeraha hilo likionekana kumuathiri na Julai nne akimaliza wa tatu katika mbio za maili kwenye Prefontaine Classic.

Matokeo hayo yalikomesha mfululizo wake wa kutoshindwa katika mbio za maili uwanjani, huku sasa Kipyegon akilenga kupona kikamilifu kabla ya kurejea katika mashindano msimu ujao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *