#Athletics #Sports

ODIRA KUKABILIANA NA MABINGWA WA ULAYA NA OLIMPIKI JIJINI ZURICH

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 Lilian Odira anakabiliwa na mtihani mzito katika mashindano ya Weltklasse Zürich Agosti 27, ambapo atakutana na bingwa wa Ulaya Audrey Werro na bingwa wa Olimpiki Keely Hodgkinson.

Odira anaingia kwenye mashindano hayo akiwa bingwa wa dunia baada ya kutwaa dhahabu jijini Tokyo mwaka 2025 kwa muda bora wa dakika 1:54.62, unaomweka katika nafasi ya nane kwa muda bora zaidi kuwahi kurekodiwa duniani.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa kivutio kikubwa baada ya Werro kumshinda Hodgkinson na kutwaa ubingwa wa Ulaya mjini Birmingham, huku Odira akilenga kuonyesha ubabe wake mbele ya wapinzani hao wakuu wa mbio za mita 800.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *