#Local News

MUTAHI KAGWE AHIMIZA KUHUSU UKULIMA WA UMUAGILIAJI MAJI

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ametoa wito wa kuharakishwa kwa upanuzi wa kilimo cha umwagiliaji nchini ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi wa mvua.

Kagwe amesema kuimarisha mifumo ya umwagiliaji ni muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha uzalishaji wa chakula hauathiriwi na ukosefu wa mvua wa kutosha.

Amesisitiza umuhimu wa serikali kuwekeza zaidi katika miundombinu ya umwagiliaji ili wakulima waweze kuzalisha chakula kwa uhakika mwaka mzima na hivyo kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *