#Local News

SAKAJA: NAIROBI INA VITANDA 43 VYA ICU KUTOKA SUFURI MWAKA 2022

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amesema kaunti hiyo imepiga hatua katika huduma za afya baada ya kuongeza vitanda vya wagonjwa mahututi ICU hadi 43 kutoka sifuri mwaka 2022.

Sakaja amesema Nairobi pia imeanza kuwa na vitengo vya kwanza vya huduma maalum kwa watoto wachanga, akisema hatua hiyo imeboresha uwezo wa kaunti kutoa huduma muhimu za afya.

Amesema fedha zinazotengwa kwa Nairobi zimeongezeka kwa asilimia 271, kutoka Shilingi milioni 700 mwaka 2022 hadi Shilingi bilioni 2.6, akisema ongezeko hilo limewezesha kuboresha huduma za kaunti.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *