TOTTENHAM YAFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI SAVINHO
Tottenham imefikia makubaliano ya awali na Manchester City kumsajili mshambuliaji Savinho, huku ada ya uhamisho ikitarajiwa kuzidi pauni milioni 75.
Savinho anatarajiwa kusafiri kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake, huku maelezo ya mwisho kuhusu ada hiyo yakisubiriwa.
Tottenham pia ina matumaini ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush, huku mazungumzo yakiwa katika hatua za juu na masharti binafsi ya mchezaji huyo tayari yakiwa yamekubaliwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































