#Football #Sports

TALANTA STADIUM KUPEWA UMEME MAALUM KABLA YA AFCON 2027

Uwanja wa Talanta utakuwa na kituo chake maalum cha umeme ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika wakati wa kuandaa mechi za AFCON 2027, Waziri wa Michezo Salim Mvurya amesema.

Mvurya amesema uwanja huo utahitaji umeme mwingi kuendesha miundombinu yake ya kisasa, hivyo ujenzi wa kituo hicho cha umeme ni muhimu kuhakikisha huduma haitaathiriwa wakati wa mashindano.

Waziri huyo amesema ana imani uwanja utakamilika kwa wakati kwa ajili ya AFCON 2027, huku uwanja wa kuchezea ukiwa tayari na kazi ikiendelea katika viwanja vitatu vya mazoezi vinavyohusishwa na kituo hicho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *