#Local News

WANDAYI: MAFUTA YA TURKANA KUANZA KUTIRIRIKA KABLA YA MWISHO WA MWAKA

Waziri wa Kawi na Petroli Opiyo Wandayi amesema Kenya inatarajia kuanza uzalishaji wa kibiashara wa mafuta ghafi kutoka Turkana kabla ya mwisho wa mwaka 2026, hatua itakayoiweka nchi katika njia ya kuanza uzalishaji wa mafuta kibiashara.

Wandayi amesema serikali imepiga hatua kubwa katika kuendeleza mradi wa mafuta wa South Lokichar kutoka hatua ya ugunduzi hadi uzalishaji wa kibiashara, huku maandalizi ya kuanza uchimbaji yakiendelea.

Amesema kuanza kwa uzalishaji kutakuwa hatua muhimu katika safari ya muda mrefu ya Kenya kuelekea kuwa taifa linalozalisha na kuuza mafuta katika masoko ya kimataifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *