NYAKERA AACHANA NA UGAVANA NAIROBI, AELEKEZA MACHO MAKADARA
Mwanasiasa wa chama cha DCP Irungu Nyakera ameondoa azma yake ya kuwania ugavana wa Nairobi katika uchaguzi wa 2027 na sasa analenga kiti cha ubunge wa Makadara
Nyakera amesema uamuzi huo umetokana na mashauriano na washauri wake wa kisiasa pamoja na shinikizo kutoka kwa wakazi wa Makadara waliomtaka kurejea katika eneo hilo na kuwania ubunge
Amesema sasa atazingatia kampeni za Makadara huku akijipanga kurejea katika eneo hilo kisiasa na kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































