POLISI WAWEKA MIKAKATI YA USALAMA WA UCHAGUZI 2027
Huduma ya Kitaifa ya Polisi imewakutanisha maafisa wakuu wa usalama na wadau mbalimbali katika kikao cha siku mbili jijini Nairobi, kinacholenga kuimarisha maandalizi ya usalama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Mkutano huo umeandaliwa na Huduma ya Kitaifa ya Polisi kwa ushirikiano na Kitengo cha Mageuzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani, huku ukisaidiwa na Ubalozi wa Uingereza pamoja na Taasisi ya Sheria za Uchaguzi na Utawala Afrika.
Polisi wamesema mkutano huo unalenga kupitia rasimu ya mpango wa maandalizi ya usalama wa uchaguzi na kutathmini hatua ambazo taasisi mbalimbali zimechukua kufikia sasa, huku mikakati zaidi ikiwekwa kuhakikisha uchaguzi wa 2027 .unafanyika kwa usalama na utulivu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































