#Football #Sports

ARSENAL YAFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI KONSA KWA £50M

Arsenal imefikia makubaliano na Aston Villa kumsajili beki wa Uingereza Ezri Konsa kwa ada ya pauni milioni 50 pamoja na malipo ya ziada, huku mkataba wa muda mrefu ukiwa tayari.

Konsa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha rasmi uhamisho wake na kutia saini mkataba wa kujiunga na Arsenal.

Hatua hiyo inaifanya Arsenal kuongeza nguvu katika safu yake ya ulinzi huku Konsa akitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya mipango ya kikosi hicho katika msimu mpya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *