#Local News

WATU 7 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA AJALI YA NDEGE SAMBURU

Ndege aina ya Helikopta imeanguka katika eneo la Mlima Ololokwe, Kaunti ya Samburu, na kusababisha vifo vya watu wote saba waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini KCAA imethibitisha ajali hiyo, ikisema ilihusisha helikopta  yenye nambari ya usajili 5Y-GYM.

Kwa mujibu wa KCAA, helikopta hiyo ilikuwa ikitoka Loisaba kuelekea Ewaso Nyiro ilipoanguka mapema leo  huku uchunguzi ukitarajiwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *