#Local News

WANAFUNZI WAWILI KERICHO WAUAWA

Familia mbili katika eneo la Koingeren, Kaunti ya Kericho, zimekumbwa na majonzi baada ya miili ya wanafunzi wawili waliokuwa wamepotea kupatikana katika shamba la miwa. Wanafunzi hao, wenye umri wa miaka 18 na 16, walikuwa hawajulikani waliko kwa siku kadhaa.

Miili yao imepelekwa katika hifadhi ya maiti kwa uchunguzi zaidi. Polisi wameanza uchunguzi ili kubaini kilichosababisha vifo vya wanafunzi hao.

Mamlaka za usalama zinaendelea na uchunguzi huku familia zikisubiri majibu kuhusu mazingira ya vifo vya wapendwa wao.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *