VIONGOZI WA SERIKALI WATAKA UPINZANI KUMHESHIMU RAIS RUTO
Sehemu ya viongozi wanaounga mkono serikali ya ushirikiano mpana imewakosoa wanasiasa wa upinzani kwa kutoheshimu uongozi wa Rais William Ruto, huku wakitetea utendakazi wake
Viongozi hao wamesema serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi
Aidha wameeleza imani kuwa Rais Ruto ataibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa 2027, wakisema wananchi wataangalia rekodi ya serikali katika kuamua viongozi wao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































