#International

HICHILEMA ASHINDA UCHAGUZI ZAMBIA KWA ASILIMIA 60

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameshinda muhula mwingine wa uongozi baada ya kupata asilimia 60 ya kura katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi iliyopita.

Uchaguzi huo ulikuwa kwa kiasi kikubwa wa amani, ingawa upinzani ulidai kulikuwa na vitisho, kukamatwa kwa wafuasi, ghasia na ukiukaji wa taratibu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.

Hichilema, aliyeingia madarakani mwaka 2021, alikuwa akikabiliana na wagombea 13 akiwemo aliyekuwa waziri wa mkoa Brian Mundubile, aliyekuwa akiwania urais kwa mara ya kwanza.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *