#Local News

RAIS RUTO ATETEA MPANGO WA AFYA YA KIDIJITALI

Rais William Ruto ametetea mpango wa serikali kueka mfumo wa afya kidijitali akisema hatua hiyo ni muhimu katika kufanikisha huduma bora za matibabu kwa wote nchini.

Akizungumza mjini Nairobi wakati wa mkutano wa kitaifa wa afya Ruto amesema technolojia hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji, kufuatilia matibabu na kuwezesha matumizi ya fedha kwa usahihi.

Aidha Rais Ruto ametumia muda huo kukiri kuwa mfumo wa SHA unavutia ukosoaji mkubwa kwa sasa japo serikali haiwezi kuyumbushwa kwa nia yake ya utoaji huduma.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *