#Local News

JAMII YA LUO KATIKA KAUNTI YA TRANS NZOIA YAKASHIFU VURUGU ZA JUMAPILI

Wazee wa jamii ya Luo katika Kaunti ya Trans Nzoia wamekashifu vurugu zilizotokea Homa Bay wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi na kuomba msamaha kwa viongozi pamoja na waathiriwa wa ghasia hizo.

Wazee hao wamesema vurugu za aina hiyo hazipaswi kuhusishwa na jamii yoyote, wakisisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za wananchi kushiriki katika shughuli za kisiasa kwa amani bila vitisho au mashambulizi.

Wamewataka viongozi na wananchi kuacha vitendo vya uchochezi na badala yake kushirikiana kulinda amani na umoja wa kitaifa, hasa wakati Kenya ikielekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *