VYAMA VYA KISIASA KUSAINI HATI YA AMANI
Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano Askofu Kepha Nyamweya amesema kila chama cha kisiasa kinatarajiwa kusaini hati ya amani kuelekea uchaguzi mkuu, hatua inayolenga kukuza utulivu na kuzuia migawanyiko ya kisiasa nchini
Nyamweya amesema pia kuna majadiliano ya kuhakikisha kila anayelenga kuwania nafasi ya kisiasa anapitia mchakato wa kuthibitishwa na NCIC, pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa
Amesema Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, huenda ikawa chombo cha mwisho kuidhinisha wagombea kabla ya kuruhusiwa kushiriki katika uchaguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































