UCHUNGU WA SUKARI WAENDELEA KUJITOKEZA
Wabunge kutoka Magharibi mwa nchi wametishia kuelekea mahakamani ili kushinikiza kubatilishwa kwa mchakato wa kukodishwa kwa kiwanda cha miwa cha Nzoia, wakidai serikali imekiuka sheria katika kumkabidhi mwekezaji wa kibinafsi usimamizi wa kiwanda hicho.
Wakizungumza na wanahabari jijini Nairobi, viongozi hao wameishutumu serikali kwa wanachosema kukosa uwazi katika mchakato huo.
Miongoni mwao ni seneta wa Vihiga Godfrey Otsotsi, Edwin Sifuna wa Nairobi na mwenzake wa Busia Okiya Omtatah na mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































