DIG LANGAT CHINI YA SHINIKIZO
Kamati ya usalama katika bunge la kitaifa imetoa shinikizo kwa naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Langat kujiuzulu kufuatia mauaji ya bloga Albert Ojwang, aliyekamatwa kwa madai ya kuchapisha taarifa za uongo kuhusu Langat kabla ya kifo chake.
Kamati hiyo imetaka kufanywa uchunguzi wa kina kuhusu mauaji hayo, ili kila afisa wa polisi aliyehusika awajibishwe kisheria, huku spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, akiiagiza kamati hiyo kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa awali hapo kesho kabla ya kikao kuhusu bajeti kuanza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































