#Football #Sports

CHELSEA WAADHIBIWA KWA MAKOSA YAO- ROSENIOR

Meneja wa Chelsea Liam Rosenior amekiri kwamba kikosi chake kiliadhibiwa kutokana na makosa yao yaliwapa Arsenal uongozi wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya dimba la Carabao Cup jana usiku baada ya kupokezwa kichapo cha mabao 3-2 nyumbani.

The Blues wana mlima wa kukwea katika mkondo wa pili watakazuru Fly Emirates tarehe 3 mwezi ujao kujaribu kuwasimamisha Arsenal katika safari ya kuelekea Wembley kupambana na mshindi kati ya Manchester City na Newcastle.

Kipa wa Chelsea Robert Sanchez alikuwa kitovu cha utepetevu, makosa mawili yakichangia mabao waliofungwa na Ben While na Viktor Gyokeres licha ya nguvu mpya Alejandro Garnacho kufunga mabao 2.

Kulingana na Rosenior, vijana wake walikosa umakini baada ya kurejea kwa kipindi cha 2.

Arsenal wamecheza mechi 10 bila kupoteza katika mashindano yote, na wananusia taji lao kuu la kwanza tangu ubingwa wa FA mwaka 2020.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CHELSEA WAADHIBIWA KWA MAKOSA YAO- ROSENIOR

ARBELOA AANZA KWA MASAIBU REAL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *