#Rugby #Sports

LIONESSES WAJIANDAA KWA MASHINDANO YA KIHISTORIA NYUMBANI

Timu ya taifa ya raga ya wanawake ya Kenya, Lionesses, iko katika hali
nzuri ya maandalizi na motisha ya hali ya juu kuelekea mashindano ya
kwanza kabisa ya HSBC World Rugby Sevens Series Tier Two
yatakayofanyika nyumbani.

Naibu meneja wa timu Peruz Muyuka amesema Lionesses
wanaimarika kutokana na uzoefu walioupata awali katika
mashindano ya World Series, hali iliyosaidia kuboresha mbinu za
kiuchezaji na mipango ya kiufundi.

Kama sehemu ya maandalizi, timu hiyo ipo nchini Uhispania kwa
kambi ya siku tano ya mazoezi ya kiwango cha juu itakayokamilika
Februari Mosi, ambapo watacheza mechi za kirafiki dhidi ya Uhispania
na Ubelgiji kabla ya kurejea nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *