#Local News

RUTO AKABILIWA NA SUALA LA MGOMO WA WAHUDUMU WA AFYA

Mkutano wa Afya nchini wa siku mbili umehitimishwa kwa wito wa kumalizwa haraka kwa mzozo kuhusu maslahi ya wahudumu wa afya ili mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo yaendelee.

Suala la uhaba na migogoro ya wafanyakazi lilitawala mjadala ulioongozwa na Rais William Ruto, huku wahudumu wa afya wanaogoma wakimweleza malalamiko yao moja kwa moja.

Hata hivyo Baraza la Magavana limepinga baadhi ya madai ya wahudumu hao, huku washikadau wakitaka suluhu ya haraka ili kurejesha huduma za afya na kuimarisha sekta hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *